advertising :- @life1Cee
Fan Channel Domelipa 💋
Last updated hace 4 días, 7 horas
Last updated hace 1 año, 1 mes
Hech kim mukammal emas...
Shuning uchun qalamlarda o'chirg'ich bor!
Last updated hace 4 días, 6 horas
📚📚📚HUKUMU YA KUWEKA MKONO JUU YA MSAHAFU NA KUAPA!!
Amesema Sheikh Sway Alfawzani -حفظه الله-:
|[ وضع اليد على المصحف والحلف لا أصل له وإنما هو من فعل العوام. |]
((Kuweka mkono Juu ya Msahafu na kuapa ni jambo ambalo halina Asili ni miongoni mwa matendo ya watu wa kawaida si wenye Elimu.))
📓| (شرح إغاثة اللهفان ١٤٣٧/١/٢٦).
✅Kiapo ni tamko la kuapa wala haifai kuapa kwa asiye kuwa Allāh,
Mfano wa kuapa ni kama kusema "Naapa kwa jina la Allāh" au kusema "Wallāhi au Wabillāhi au Watallāhi"
Au kuapa kwa sifa ya Allāh iliyo egemezwa kwa Allāh mfano ukasema "Naapa kwa Elimu ya Allāh au Nguvu na Uwezo wa Allāh" n.k
Ukishatamka tu umekwisha hiyo kiapo kishapita haihitaji ushike Msahafu wala upitishe kidole cha shahada shingoni!!
Wala si katika kiapo maneno haya wengi hupenda kuyatumia "Haki ya Mungu na Mtume"!!
والله أعلم.
🪐🔥🪐 #HIZBU_MAFUTA WANALAZIMISHA KUTUITA #HAJAAWERA KWA DHULMA ILI HALI SIE SIO WAFUASI WA SHEIKH YAHYA حفظه الله تعالى !!
Amesema Sheikh Rabiī Al-madkhaliy حفظه الله تعالى:
فأهل السنة لا ينتسبون إلا للكتاب والسنة لا ينتسبون إلى فلان وفلان، ويحاولون أن يرمونا بهذه الألقاب، وهابي، جامي، فلان ...هذا كذب نحن دعاة إلى كتاب الله وإلى سنة رسول اللهﷺ .
((Hakika Ahlu Sunna hawajinasibishi na chochote Ispokuwa Kitabu na Sunna kamwe hawajinasibishi na Mtu Fulani na Fulani,
Lakini watu wa batili wanajaribu kutunasibisha Sisi na Lakabu hizo WAHABI mara JAMIY mara (HAJAAWERA)!!
Huu wote ni Uongo Sisi ni Walinganizi kuelekea kwenye Kitabu cha Allāh na Sunna za Mtume ﷺ.))
المجموع ج15 ص186
🚥🌿🚥FADHILA YA KUSAMEHE NA KUSAMEHEANA NA NYOYO KUWA SAFI NA KUNJUFU!!
Kutoka kwa Abu Hureyrah رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ ,
kutoka kwa Mtume صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ amesema :
(( مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِلَّا عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلَّا رَفَعَهُ اللَّهُ ))
|{Swadaka haijawahi kupunguza Mali na Allāh hakumzidishia Mja kwa Kusamehe ila Utukufu na hakujishusha yoyote kwa ajili ya Allah ila Allāh humnyanyua.}|
📚 صحيح مسلم - رقم : (2588)
Kutoka kwa Abu Hureyrah رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ ,
Hakika Mtume صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ amesema :
(( تُفْتَحُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ يَوْمَ الِاثْنَيْنِ وَيَوْمَ الْخَمِيسِ، فَيُغْفَرُ لِكُلِّ عَبْدٍ لَا يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا، إِلَّا رَجُلًا كَانَتْ بَيْنَهُ وَبَيْنَ أَخِيهِ شَحْنَاءُ، فَيُقَالُ : أَنْظِرُوا هَذَيْنِ حَتَّى يَصْطَلِحَا، أَنْظِرُوا هَذَيْنِ حَتَّى يَصْطَلِحَا، أَنْظِرُوا هَذَيْنِ حَتَّى يَصْطَلِحَا ))
[{Milango ya Pepo hufunguliwa siki ya Jumatatu na Alhamisi husamehewa kila Mja ambae hakumshirikisha Allāh na chochote ila Ispokuwa Mtu ambae kati yake Yeye na Ndugu yake kuna #Ugomvi!!
Husemwa;
Waacheni Hawa wawili kwanza Mpaka wasuluhishane!!
Waacheni Hawa wawili kwanza Mpaka wasuluhishane!!
Waacheni Hawa wawili kwanza Mpaka wasuluhishane!!}]
📚 صحيح مسلم - رقم : (2565)
✅ Amesema Sheikh Ibn Baz رحمه الله :
هذا يَدُلُّ على أَنَّ الشَّحناء مِن أسبابِ إيقافِ المغفرةِ عن المُتَشَاحِنِين، وهذه مُصِيبَةٌ كَبِيرَة، فالواجبُ على كُلِّ مُؤْمِنٍ أَنْ يَحرِصَ على المَحَبَّةِ لِأَخِيهِ وَالصُّلْحُ مَعَ أَخِيهِ، وَعَدَم الشَّحنَاء، تحلّ المشاكل بِالطُّرُقِ الطَّيِّبَةِ وَالتَّسَامُحِ لا بِالشَّحنَاءِ ولا بِالتَّهَاجُر .
((Hii inaonesha kwamba Ugomvi ni sababu ya kuzuiya Maghfira kati ya wale wenye kugombana,
Na huu hakika ni Msiba ulio mkubwa,
Jambo la wajibu kwa kila Muumini ni kwamba awe na Pupa juu ya kumpenda Ndugu yake na kufanya Suluhu na Ndugu yake na kusiwe na Chuki na Ugomvi,
Hivyo mizozo yote itatuliwekwa Njia nzuri kwa kusameheyana Si kwa Ugomvi wala kuhamana.))
📚 شرح رياض الصالحين : (313/4)
√|📂|√ WINGI KATIKA SWALA YA JENEZA NI KATIKA MAMBO MUHIMU..!!
Kutoka kwa Mama Ãishah رَضِيَ اللهُ عَنْهَا amesema:
Amesema Mtume ﷺ :
|[ما من ميِّتٍ تُصلِّي عليه أمَّةٌ من المسلمين يبلغون مِئَةً . كلُّهم يشفعون له . إلَّا شُفِّعوا فيه |]
((Hakuna Maiti akaswali na kundi la Waislamu wanao fika mia Moja wote wakimfanyia uombezi ila Ispokuwa Uombezi wao utakubaliwa juu yake.))
📓| (رواه مسلم ٩٤٧).
🤲Yaa Allāh tuwafikishe.
???? KATAZO LA WAISLAMU KUVAA NGUO IKAVUKA VIFUNDO VIWILI VYA MIGUU!!
Kutoka kwa Abu Hureyrah رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، Kutoka kwa Nabii صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ amesema :
(( مَا أَسْفَلَ مِنَ الْكَعْبَيْنِ مِنَ الْإِزَارِ فَفِي النَّارِ ))
[|{Kile kilichozidi kongo mbili katika nguo ni Motoni ?.}|]
? صحيح البخاري - رقم : (5787)
2 - Kutoka kwa Abdullāhi bin Omar رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا ، amesema :
Amesema Mtume صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :
(( مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلَاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللَّهُ إِلَيْهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ))
[{Mwenye kuburuza Nguo yake kwa #Kibri hakika Allāh hatomtazama siku ya Kiama.}]
? متفق عليه : (3665-2085)
✍ Hadithi ya kwanza inaonesha hukumu ya mwenye kuvaa nguo yake Ikavuka kongo mbili na,
Hadithi ya pili inaonesha hukumu ya mwenye kuburuza Nguo yake kwa kibri
Hii inaonesha kwamba hukumu ya ((ISBALI)) yaani Kuvaa nguo ikazidi kongo mbili haiko katika daraja Moja;
Bali Kuna kuvaa nguo ikazidi kongo mbili na Kuna kuiburuta nguo kwa kibri na fakhari hii inakuwa imebeba mambo mawili kwa pamoja,
Tahadhali zinduka.
??? KATAZO LA KUNYOA MTINDO WA PANKI AU DENGE BALI IMA UNYOE ZOTE AU UACHE ZOTE!!
Kutoka kwa Ibn Omar رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا ، amesema :
(( سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْهَى عَنِ الْقَزَعِ ))
Hakika Nilimsikia Mtume ﷺ akikataza ((kaza'ā)) !!
Akasema Nafi'ī:
يُحْلَقُ بَعْضُ رَأْسِ الصَّبِيِّ، وَيُتْرَكُ بَعْضٌ
Ni Kunyoa nywele za Mtoto baadhi na ukaacha baadhi .
? متفق عليه : (5920-2120)
advertising :- @life1Cee
Fan Channel Domelipa 💋
Last updated hace 4 días, 7 horas
Last updated hace 1 año, 1 mes
Hech kim mukammal emas...
Shuning uchun qalamlarda o'chirg'ich bor!
Last updated hace 4 días, 6 horas