سلفيون في كينيا

Description
كلمات
دروس
محاضرات
ردود العلمية
Advertising
We recommend to visit

Last updated hace 1 año, 1 mes

🇺🇿 SUMDA DONAT: https://idonate.uz/d/mashatoga
🦄TRIKCHILIK: https://tirikchilik.uz/MASHATOGA
💸 DONAT RUB: https://www.donationalerts.com/r/mashtoga
Youtube: https://youtube.com/@MASHATOGA
UC UCHUN - @NINJA_WINN

Last updated hace 2 semanas

كلمات
دروس
محاضرات
ردود العلمية

Last updated hace 1 mes, 1 semana

1 month, 1 week ago
1 month, 1 week ago

بسم الله الرحمن الرحيم

🌴 UWANJA WA MASJID- TAWHEED 🌴

🍂MUTHAIGA, NANYUKI🏔️,KENYA 🇰🇪.🍂

خطبة عيد الأضحى

🔊KHUTBAH YA EIDUL ADH'HAA:

💺KHATWIIB🎙

AL AKH ABUU ZUBEIR SULEIMAN (حفظه الله ورعاه)•

🗓 JUMAMOSI;TAREHE:1⃣0⃣,DHUL HIJJAH 1⃣4⃣4⃣5⃣H.
SAWA NA:1⃣6⃣/0⃣6⃣/2️⃣0⃣2⃣4⃣M•

🗯TUNAKUNASIHINI KUISKIZA NA KUITAWANYA🗨•

https://t.me/sautiyat

Telegram

سلفيون في كينيا

كلمات دروس محاضرات ردود العلمية

بسم الله الرحمن الرحيم
1 month, 1 week ago
1 month, 1 week ago

بسم الله الرحمن الرحيم

❇️•MASJID TAWHID,MUTHAIGA•❇️

NANYUKI, KENYA 🏔

🔊 KHUTBAH YA IJUMAAH KWA 
           UNWAAN

▫️FADHILA ZA SIKU YA ARAFAH•

_YALIYOMO_

🔖MASAIL NA AHKAM KUHUSIANA NA UDHHIYA•

🗓IJUMAAH; TAREHE 0⃣8️⃣
      DHUL HIJJAH 1⃣4⃣4⃣5️⃣H
                 SAWA NA
1️⃣4️⃣/0️⃣6⃣/2️⃣0⃣2⃣4️⃣M•

🗯TUNAKUNASIHINI KUISKIZA NA KUITAWANYA🗨•

💺KHATWIIB🎙

AL AKH ABUU ZUBEIR SULEIMAN (حفظه الله ورعاه)•

https://t.me/sautiyat

Telegram

سلفيون في كينيا

كلمات دروس محاضرات ردود العلمية

بسم الله الرحمن الرحيم
1 month, 2 weeks ago

'The Blessing Of Eemaan And Means Of Strengthening It In These Ten Days Of Dhul-Hijjah'

Abuu Fajr 'Abdul-Fattaah Ibn 'Uthmaan, may Allaah preserve him

30th Dhul-Qi'dah 1442 - 10/07/2021

Masjid Al-Istiqama
Toronto, Canada

For more beneficial audios: t.me/SalafiSermons

Join us on https://t.me/Jannah_Is_Our_Dream

1 month, 2 weeks ago

**قال سهل بن عبدالله التستري:

(شكر العلم: العمل؛ وشكر العمل: زيادة العلم).

[حلية الأولياء ١٣/١٩٤]**

Sahl bin Abdullah At-Tustari amesema:

(Shukrani ya elimu ni àmal;na shukrani ya àmal ni kuzidisha elimu).
[Hilyat Al-Awliya’ 13/194]

https://t.me/madaarijus_Saalikin

1 month, 3 weeks ago

Yaani, yeye anajitakasa na kila fujo na matusi dhidi ya markaz Dammaaj na dhi

1 month, 3 weeks ago

*Anasema, yeye alikuwa na ukaribu sana kwao mpaka hata alikuwa ndiye wa kati baina ya wanafunzi wa Jazaa-ir na kundi la Abdu Rahman al Adaniy, na walikuwa hawawezi kumsajili mwanafunzi yeyote wa Jazaa-ir ila yeye -Uthmaan- akimwadilisha na kusema yuko sawa. Na iwapo atamjeruhi mtu na kumtahadharisha kwao, walikuwa wanatahadhari naye, na hawawezi kumsajili. Na Uthman alipokuwa akienda kwao na baadhi ya wanafunzi wa Jazaa-ir, wanamuuliza hali yake kwa kutumia ishara. Ndio maana wakati Shaikh Yahya aliwaita Yaasin al Adaniy, Naaswir al Adaniy na Abul Khathwaab Alliibiy (na hawa watatu ni miongoni mwa watu wa shari sana katika fitna hio), na kuwauliza kuhusiana na kadhia hio, walimwambia Shaikh, "lakini wewe huna dalili kuwa sisi ni wahusika", kwa kuwa hawakufaa kumwambia yeyote mambo yao, isipokuwa wale ambao  wako pamoja nao kwa fikra yao.

Hata hivyo, Shaikh mwishowe aliwajua, na wengi tuu katika watu hawa wa fitna waliweza kutimuliwa Dammaaj, hasa huyu Yaasin al Adaniy ambaye alikuwa anamchukia Shaikh sana, mpaka aliwahi kutamka kwa kinywa chake kuwa anamchukia sana Shaikh, mpaka hata hataki kumwangalia usoni. Hio ni wakati aliambiwa mbona asimshukuru Shaikh Yahya kwa kuwa amemwekea utangulizi katika kitabu chake. Hivi ndivyo uhizbiyya unavyomfanya mtu mpaka anakaribia kuungua moyoni kutokana na chuki yake kwa Ahlul Hadiith. Yaasin huyu hata kuna wakati Shaikh alikuwa mgonjwa, bwana mmoja  alipomwambia kuwa Shaikh ni mgonjwa, alisema, "namwomba Allaah amwangamize", kwa kuweka haraka ya dhwammah kwa herufi ya yaa, katika neno "yashfiyahuu, yeye akasema, yushfiyahuu." Yaani, "أسأل الله أن يشفيه", kisha wote wawili wakacheka! Na katika maneno yake, aliwahi kusema kuwa mwambieni Shaikh Yahya aweke kipindi cha kuuliza maswali kiwe baada ya darsa, kisha akasema, lau kama wao -yaani Shaikh Yahya na Shaikh Jamiil ambaye alikuwa naibu wa Shaikh- wangejua kiwango chao (cha elimu), hawangerefusha darsa! Huyu Yaasin, kulikuwa na uadui mkali baina yake na Abdu Rahman al Adaniy mwanzoni, kabla ya fitna hii.

Shaikh Kamaal bin Thaabit -Allaah amrehemu- katika kitabu chake "حقائق وبيان" anaelezea kuwa siku moja akiwa anaelekea msikitini kwa ajili ya kuhudhuria darsa baada ya dhuhr, Abdu Rahman alimuita na kumwambia, huyu -Yaasin- hana adabu, na sidhani kama amewafikishwa! Ila angalia baada ya fitna wameungana na kuelewana, kwa kuwa wote wawili wako dhidi ya Shaikh Yahya. Na Shaikh Yusuf anataja habari ya Amiin al Khaarifiy ambaye alikuwa mmoja wao na kisha akaachana na wao na kutoa siri yao, na jinsi watu hao walivyokuwa wakifanya Dammaaj kipindi hicho cha tasjiil. Anasema, watu wa Abdu Rahman al Adaniy walikuwa wakiwapigia simu wale ambao wamemakinika katika elimu na Da'awah, na kuwalalamikia kuwa Shaikh Yahya kafanya hivi, na kadhalika. Na walikuwa wakimzungumzia kwa ubaya Shaikh na mtu yeyote ambaye yuko karibu na Shaikh, mpaka wakawa wakisema kuwa Shaikh Kamaal al Adaniy -kwa kuwa hakuwa pamoja nao- eti anataka Abdu Rahman aanguke, ndio yeye awe juu.

Na walikuwa wakitafuta huruma kwa watu kwa kuwaambia kuwa Abdu Rahman anadhulumiwa na Shaikh Yahya, mpaka wakafanya baadhi kumchukia Shaikh Yahya kwa ajili hio, na kuwahamasisha dhidi ya Shaikh kwa kuwaambia, kuweni wenye kumnusuru Abdu Rahman. Mpaka wakawaambia watu wao wapeleke malalamishi kwa mashekhe wengine wa Yemen, na eti mtu mgeni anayekuja Dammaaj huwa anaulizwa na Shaikh Yahya jee yeye ako na nani katika fitna hii, akisema ako na kina Abdu Rahman, anafukuzwa, na huu ni uongo. Katika vikao vyote vitatu ambavyo mashekhe wa Yemen walikaa na kumtaka Abdu Rahman aache tasjiil -ya kwanza ilikuwa Dammaaj, ya pili Ma'abar kwa Muhammad Imaam, na ya tatu Hudeidah kwa Muhammad Waswaabiy- walimnasihi Abdu Rahman aachane na genge lake ambalo kazi yao ilikuwa kumtukana Shaikh Yahya na kumzungumzia kwa ubaya. Angalia kwa mfano katika kikao hicho cha Hudeidah, Abdu Rahman mwenye aliyaandika maneno yafuatayo,

"فإني أبرأ إلى الله تعالى من كل إثارة وطعن ضد مركز دماج وضد الشيخ يحيى ومن فعل شيئا من ذلك فإنما يمثل نفسه ولا يمثلني."*

1 month, 3 weeks ago

*Na kulikuwa na matendo mengi ya kihizbi waliyokuwa wakiyafanya, mpaka wakawa wenye kuwakata ndugu zao na kuwahama, ilhali wote wako katika markaz moja,  na chini ya Shaikh mmoja! Abdu Rahman al Adaniy mwenyewe alikuwa akiwakata na kuwahama hata mashekhe ambao wako karibu na Shaikh Yahya, kama Shaikh Sa'iid bin Da'as, na aliposalimiwa na Hamuud al Waayiliy, alinung'unika na kurusha mikono, na hio ilikuwa ndani ya Ramadhwan, kama anavyoelezea Shaikh Kamaal katika risala yake "حقائق وبيان". Na Shaikh Kamaal pia ni miongoni mwa watu ambao Abdu Rahman al Adaniy aliwakasirikia kwa fitna hio, kwa kuwa alikuwa karibu na Shaikh Yahya. Sasa Shaikh Kamaal akikutana naye njiani na kumsalimia, anajibu salamu kwa hasira, na wakati mwingine hajibu salamu. Na katika matusi ya Abdu Rahman kwa Shaikh Yahya, Shaikh Kamaal anaelezea wakati Shaikh Yahya alimtumia Abdu Rahman baadhi ya wanafunzi wampe nasiha ya kuacha kuwasajili wanafunzi, miongoni mwao akiwemo Shaikh Thwaariq Ba'adaaniy na Shaikh Muhammad Siwariy. Baada ya kunasihiwa, uso wake ukawa mwekundu, na akasema kwa hasira, "hizi ni ujinga gani, ni kama amewakinaisha -yaani Shaikh Yahya- na  kuwaathiri." Na Shaikh Kamaal ametaja pia ushahidi wa Hamuud al Waayiliy, wakati mmoja alipotoka na Abdu Rahman msikitini baada ya swalaatu dhuhri, kisha walipofika mbele ya nyumba ya Swaadiq Abdiiniy, na ameelezwa kuwa Shaikh Yahya amewazungumzia baadhi ya mashekhe, Abdu Rahman akasema eti Shaikh Yahya amewakufurisha! Yeye akamjibu, hapana, ni naswiha tuu amewapa. Na maneno ya bathwil ambayo Abdu Rahman aliyazungumza dhidi ya Shaikh Yahya ni mengi tuu, na haya ni baadhi ya mifano.

قال الشيخ زيد بن محمد المدخلي رحمه الله تعالى في خصائص علماء السنة: "الرابعة، وضوح الانطلاق والسير في عمل الدعوة إلى الله والأمر بالمعروف والنهي عن المنكر فلا سرية ولا تكتلات مخفية، ولا تجمعات خاصة في غياهب الظلام في فوات الأرض أو تحت كهوف الجبال كما يفعله الحزبيون الحركيون في كل بلد من بلدان المسلمين." قطوف من نعوت السلف ص ٩.

Mwanachuoni huyu wa Sunnah -Shaikh Zaid al Madkhaliy- alipokuwa akitaja sifa za wanachuoni wa Sunnah, anasema katika sifa hizo ni njia yao yenye uwazi wanapolingania watu kwa kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu, na hawawi wenye kufanya mambo kwa kujificha na kujigawa gawa kwa siri, wala hawawi wenye kujificha misituni, mapangoni na milimani, kama wanavyofanya "wanaharakati" na mahizbi katika kila sehemu na nchi za Kiislamu. Na Shaikh Ahmad bin Yahya Najmiy -Allaah amrehemu- alipoulizwa kama kuwachukua vijana na kukaa nao kwa sehemu za siri ni katika manhaj na njia ya Ikhwaanul Muslimiin, Shaikh alijibu kuwa ni katika njia yao. Kwa nini wajifiche iwapo yale ambayo wanafanya ni haki? Mbona wasikae misikitini? Angalia kitabu chake "الفتاوى الجلية" Uk 64.

وقال الشيخ عبد السلام بن برجس رحمه الله تعالى: "وقد حذر السلف من الاجتماعات السرية لأنها نواة الضلالة، إذ الضلالة أول ما تخرج في الأمة تكون سرا بين أناس جليسهم الشيطان يزين لهم سوء أعمالهم، ويلهمهم أن الصواب معهم دون غيرهم، وأن غيرهم عدو لما وصلوا إليه مما يعتقدون أنه الحق. وعلامة أهل الباطل الاجتماعات السرية، إذ لو كانوا على حق لما استخفوا عن أعين الناس.." الأمر بلزوم جماعة المسلمين ص ٨١-٨٥

Shaikh Abdu Salaam bin Barjas -Allaah amrehemu- anatufaidisha kuwa wema waliotangulia walikuwa wakitahadharisha watu na vikao vya siri, kwa kuwa vikao hivyo ndivyo mbegu ya upotevu. Upotevu mwanzoni unapojitokeza, huwa kwa siri, baina ya watu fulani ambao Shetani huwapambia matendo yao, mpaka wanakuwa wenye kudhania wao ndio wapo katika haki, na -wanadhania- wengine wamekuwa maadui wao baada ya wao kufikia kwenye jambo lao ambalo wao wanaona ni haki. Shaikh anasema, "alama na ishara ya watu wa bathwil ni vikao vya kisiri, kwani lau wangekuwa katika haki, hawangejificha watu wasiwaone."  Na Shaikh Yusuf al Jazaa-iriy katika kitabu chake "نصب المنجنيق" uk 77, ananukuu kutoka kwa Uthmaan al Jazaa-iriy ambaye alikuwa miongoni mwao (watu wa Abdu Rahman al Adaniy), akielezea jinsi gani walivyokuwa wakifanya mambo yao kwa siri.*

1 month, 3 weeks ago

*وقال عبد الرحمن العامري في الشيخ يحيى: "متعجل، غير متثبت، يحب التزعم والترؤس، له أغراض شخصية في إحداث فتنة عبد الرحمن العدني، حاسد على عبد الرحمن العدني، بطانته بطانة سوء، قليل التجربة في الدعوة، مستكبر، لا يقبل الحق، بذيء اللسان، سفيه، رأس الفتنة ومؤججها، من أكبر الساعين فيها، لعان، سباب، شتام، فاحش، طليق اللسان، ذو لسان عوجاء، فاجر، كذاب، بل فاق البكري في الغلو والكذب والطعن في العلماء، ربما لجأ إلى القتال، باغي، ظالم، مماري، عنده أخطاء عقدية، غال في نفسه، لا يعرف قدر العلم، لا يعرف قدر الأخوة، عديم الحلم والأناة، عديم الرفق، عديم الصبر، مفتر، ومتنقص للعلماء، ومفتر للعلماء، ومحتقر للعلماء، شابه أهل البدع، بل شابه حماد بن سليمان والزمخشري، شق الصف، وثب إلى كرسي الإمام الوادعي، ولم يتنزه من السباب والشتام، جاهل."

Angalia matusi yote haya ya huyu Abdu Rahman al 'Aamiriiy, eti Shaikh Yahya ni mwenye kuharakisha -katika kadhia na kutoa hukmu- bila kuhakikisha, eti anapenda uongozi, eti ako na matakwa yake ya kibinafsi na malengo yake kwa kuleta fitna ya Abdu Rahman al Adaniy na anamhusudu.

Eti Shaikh Yahya anakaa na marafiki waovu, na hana tajruba na ujuzi katika Da'awah. Eti yeye ni mtu mwenye kiburi na asiyekubali haki, mwenye ulimi mchafu, mpumbavu, kichwa cha fitna na mwenye kuchochea. Eti yeye ni mwenye kuwalaani na kuwatukana watu, mwenye ulimi uliopinda, muovu, muongo hata mpaka amemshinda Swaaleh Bakriy katika kuvuka mpaka na kusema uongo na vilevile kuwatukana wanachuoni. Huenda hata akafikia kwa kupigana, mwenye kukiuka mipaka, mtu mwenye dhulma, mwenye kubishana sana. Eti yuko na mukhalafa ya 'Aqiidah, mwenye ghuluw kwa nafsi yake, hajui umuhimu wa elimu wala undugu, hana upole wala utulivu, hana subra, mwenye kuwasingizia watu, mwenye kuwakosea adabu wanachuoni na kuwasingizia, na vilevile kuwadharau. Eti anafanana na watu wa bid'aa, bali anafanana na Hammaad bin Suleimaan na Zamakhshariy. Eti Shaikh ni mwenye kupasua na kugawa safu -kuwatenganisha watu- na eti alirukia kiti cha Imaamul Waadi'iy, na hajajitakasa kutokana na matusi, naye ni mjinga (hana elimu).

وقال باسل اللحجي العدني: "الشيخ يحيى منافق."

Angalia huyu anayeitwa Baasil anasema eti Shaikh Yahya ni munaafiq.

وقال علي عسعوس لحيدرة عزب: "الشيخ يحيى عنده أمور ردة."

Na huyu anasema kuwa Shaikh Yahya ako na mukhalafah zinazomtoa mtu katika Uislamu.

وقال بشير الحازمي -كما نقله عنه سميح بن علي بن قاسم أبو حمراء-: "-يحيى الحجوري- كاذب، فاجر فاسق سليط اللسان زنديق."

Huyu anasema kuwa Shaikh Yahya ni muongo, muovu, mwenye ulimi mrefu na wa kuwazungumzia watu, na zindiki (ambaye ameritadi). Na hakuishia hapo, alikuwa akiwaambia wanafunzi wa Shaikh Yahya kuwa nyinyi mtabidiishwa na kukufurishwa, nyinyi ni Khawaarij, Raafidhah na Mu'utazilah.

وقال أبو قيس خيري الليبي: "والله إن الحجوري أضر من إبليس على الدعوة السلفية."

Huyu anaapa kuwa Shaikh Yahya ni mwenye madhara makubwa kwa Salafiyyah, hata kuliko Ibliis!

وقال صالح البرقي: "الحجوري أصبح الآن يسلك مسلك الجوسسة."

Na huyu hapa anasema kuwa Shaikh Yahya ameshika njia ya majasusi.

وقال: الحجوري من خالفه في رأيه فهو مطرود، من خالفه في رأيه فهو حزبي، أقسم بالله إن هذا هو منهج إخواني."

Alisema vilevile kuwa Shaikh Yahya humfukuza yeyote ambaye anatofautiana naye katika rai, na mwenye kumkhalifu katika rai yake basi anamwita hizbiy. Kisha anaapa eti hii ndio manhaj ya Ikhwaanul Muslimiin.

قال الإمام ابن القيم رحمه الله تعالى في شأن أتباع الرسل عليهم الصلاة والسلام: "فليس للمبطلين عليهم سبيل البتة لكن بالافتراء والتلبيس والكذب والألقاب الذين هم أحق بها وأهلها دونهم." الصواعق المرسلة ٢/٧٣٧

Imaam Ibnul Qayyim anasema, "watu wa bathwil hawana njia yoyote ya kupambana na watu wa haki, ila kwa kuwasingizia, kugeuza uhalisia, kusema uongo na kuwatungia majina ambayo wao wenyewe ndio wanastahiki kuitwa kwayo.

Hayo matusi yote ni kwa sababu tuu Shaikh Yahya aliwatahadharisha na mwenendo huo, na walikuwa hata wakikosa kuhudhuria darsa za Shaikh ambazo kila mmoja anatakiwa kuhudhuria, na kukeka vikao vya siri manyumbani na hata misutini, tena vikao vya mchana na hata usiku wa manane, na baadhi wakiingia kwa manyumba kwa kujificha wasiwe wenye kuonekana.*

We recommend to visit

Last updated hace 1 año, 1 mes

🇺🇿 SUMDA DONAT: https://idonate.uz/d/mashatoga
🦄TRIKCHILIK: https://tirikchilik.uz/MASHATOGA
💸 DONAT RUB: https://www.donationalerts.com/r/mashtoga
Youtube: https://youtube.com/@MASHATOGA
UC UCHUN - @NINJA_WINN

Last updated hace 2 semanas

كلمات
دروس
محاضرات
ردود العلمية

Last updated hace 1 mes, 1 semana